Asili ya Muziki - Remy Ongala

 Muziki asili yake wapi ee

[what is the origins of music]

Muziki ni wa nani ee

[who is the owner of music]

Muziki hakuna mwenyewe

[music has no owner]

Muziki ni mwito

[music is a calling]

Muziki ni fundisho

[music is a lesson]

Muziki maombolezo kilio

[music is mourning]


Usinione nikiimba

[do not see me singing]

Ukadhani ninayo furaha

[and assume i am happy]

Kumbe ninayo huzuni moyoni

[yet i have sadness in my heart]


Muziki ilivyo na nguvu ulimwenguni kote

[music has power all over the world]


Hata makanisani wanaimba 

[even in churches they sing]

Kwa kumuabudu mungu

[to worship God]

Kwa kumsifu mungu

[to praise God]


Hata kukiwa sherehe za serikali

[Even during government functions]

Mbele ya mwenyekiti kuhutubia ee

[before chairman address gathering]

Ni muziki unaanza kuwakusanya watu

[its music that brings people together]


Kumbuka Paula na Sila 

[Remember Paul and Silas]

waliimba gerezani mungu amewasikia

[they sang in prison and God heard them]

Kumbuka Musa aliimba muziki wa aina yake

[Remember Moses sang a unique song]

Kuwakomboa wana Israeli

[to liberate the children of Israel]

Walioko utumwani katika nchi ya Misri

[who were in bondage in Egypt]


Ukiwa na sherehe 

[if you have a celebration]

utaimba nyimbo za furaha

[you will sing happy songs]

Ukiwa na taabu 

[if you have problems]

utaimba nyimbo za masikitiko

[you will sing sad songs]

Ukifa leo 

[if you die today]

utapelekwa kaburini 

[you will be taken to the grave]

na nyimbo za maombolezo

[with mourning songs]


Ni muziki pekee uliyo na nguvu

[it is only music that has power]

Itawakusanya wabaya na wazuri

[it will bring together bad and good people]

Siku ya mwisho mungu akitoa hukumu

[on the day of judgement]

Hukumu

[judgement]


Muziki sio uhuni

[music is not criminal]

Kama muziki ni uhuni

[if music was criminal]

Kwanini unanunua kaseti

[why do you buy cassete]

Kama muziki ni uhuni

[if music was criminal]

kwa nini unaomba nyimbo redioni

[why do you make requests on radio]

Kanma muziki ni uhuni

[if music was criminal]

kwa nini unanunua rekodi

[why do you buy gramophones]

Kama muziki ni uhuni

[if music was criminal]

kwa nini unacheza muziki wee

[why do you play music]

kama muziki ni uhuni

[if music was criminal]

Kwa nini unafanya top ten show

[why do you make top ten shows]


Kumbuka siku ya mwisho ikifika ee

[remember on judgement day]

Kutakuwa mlio mmoja wa parapanda

[there will be a loud trumpet sound]

Itawakusanya wateule wote

[that will bring together all the chosen]

Walioteuliwa katika pembeni za dunia

[chosen from all corners of the world]

Siku ya mwisho mungu akitoa hukumu

[On judgement day]

hukumu

[judgement]


Hata kwa mungu malaika wanaimba oo

[even in heaven the angels are singing]


Muziki asili yake wapi ee

[what is the origins of music]

Muziki ni wa nani ee

[who is the owner of music]

Muziki hakuna mwenyewe

[music has no owner]

Muziki ni mwito

[music is a calling]

Muziki ni fundisho

[music is a lesson]

Muziki maombolezo kilio

[music is mourning]


Usinione nikiimba

[do not see me singing]

Ukadhani ninayo furaha

[and assume i am happy]

Kumbe ninayo huzuni moyoni

[yet i have sadness in my heart]


instrumental


Muziki asili yake wapi ee

[what is the origins of music]

Muziki ni wa nani ee

[who is the owner of music]

Muziki hakuna mwenyewe

[music has no owner]

Muziki ni mwito

[music is a calling]

Muziki ni fundisho

[music is a lesson]

Muziki maombolezo kilio

[music is mourning]


Usinione nikiimba

[do not see me singing]

Ukadhani ninayo furaha

[and assume i am happy]

Kumbe ninayo huzuni moyoni

[yet i have sadness in my heart]

https://www.youtube.com/watch?v=iXV1u-VJrg8


Comments